Kikaidipang ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wakaidipang na Wabolaang-Itang kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kikaidipang imehesabiwa kuwa watu 26,600, yaani Wakaidipang 8900 na Wabolaang-Itang 17,700. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikaidipang iko katika kundi la Kifilipino.